1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bemba akamatwa.

Mtullya, Abdu Said25 Mei 2008

Aliekuwa makamu wa rais nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Jean-Pierre Bemba amekamatwa mjini Brussels.

https://p.dw.com/p/E5ZS
Aliekuwa makamu wa rais nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Jean-Pierre Bemba.Picha: AP


Aliekuwa makamu wa rais nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Jean -Pierre Bemba amekamatwa

Bemba ambae pia alikuwa kiongozi wa waasi alikamatwa karibu na mji mkuu wa Ubelgiji Brussels jana kutokana kufuatia ombi la mahakama ya kimataifa inayopambana na uhalifu ICC ya mjini the Hague.

Mwendesha mashataka wa mahakama hiyo ameliambia shirika la habari la AFP, kuwa mahakama ya ICC sasa inaisubiri serikali ya Ubelgiji itoe amri ili mwanasiasa huyo apelekwe mjini The Hague kujibu mashtaka manne juu ya uhalifu wa kivita na mawili ya uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Mnamo miezi ya hivi karibuni Bemba alikuwa anaishi katika hifadhi ya kisiasa nchini Ureno baada ya kushindwa katika uchaguzi wa rais nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo miaka miwili ilyopita.

Bemba pia anakabiliwa na shtaka la uhaini nchini mwake.