1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bemba asema bado harejei Kongo

9 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D4to

Lisbon:

Makamo wa rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Jean Pierre Bemba,anaeishi hivi sasa nchini Ureno,ameondowa uwezekano wa kurejea nyumbani kwa sasa.Akizungumza na shirika la habari la Ureno-Lusa ,Jean Pierre Bemba amesema "sababu za usalama ndizo zinazomzuwia kurejea nyumbani kwa sasa."Ameituhumu serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kutobuni hali itakayomrahisishia kurejea nyumbani.

Gazeti la "Le Palmares liliripoti hapo awali kwamba Jean-Pierre Bemba,mwenyekiti wa chama cha waasi wa zamani cha ukombozi wa Kongo-mgombea aliyeshindwa wa uchaguzi wa rais,october mwaka 2006 anapanga kurejea nyumbani mapema mwezi ujao.Jean Pierre Bemba anaishi Ureno tangu April mwaka jana kwa sababu za matibabu.