1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ben Ali na mkewe waadhibiwa miaka 35

21 Juni 2011

Mahakama nchini Tunisia, imetoa hukumu ya kifungo cha miaka 35 kwa rais wa zamani Zine al-Abidine Ben Ali.

https://p.dw.com/p/RUqT
Judge Touhami Hafi gestures, at the Tunis Criminal Court, in Tunis, Monday, June 20, 2011, for the hearing of the two embezzlement cases of money laundering and drug trafficking, against Zine El Abidine Ben Ali , Tunisia's former autocratic ruler. Tunisia's former autocratic ruler, whose ouster triggered a series of Arab world uprisings, went on trial in absentia Monday in the first of what will likely be a long series of court proceedings five months after he went into exile. The Tunis Criminal Court is hearing two embezzlement, money laundering and drug trafficking cases against Zine El Abidine Ben Ali. It follows the discovery of around $27 million in jewels and cash plus drugs and weapons at two palaces outside Tunis after he flew to Saudi Arabia on Jan. 14. Ben Ali, 74, vigorously denied the charges in a statement through his French lawyer, calling the proceedings a "shameful masquerade of the justice of the victorious." (Foto:Hassene Dridi/AP/dapd)
Jaji Touhami Hafi katika kesi ya Ben Ali mahakamani TunisPicha: AP

Hukumu hiyo imetolewa wakati akiwa Saudi Arabia alikokimbilia, tangu miezi sita iliyopita, kufuatia mapinduzi yaliyochochea vuguvugu la kidemokrasia katika ulimwengu wa Kiarabu. Katika kesi iliyosikilizwa siku moja, rais wa zamani wa Tunisia, Ben Ali amekutikana na hatia ya wizi na kumiliki vyombo vya dhahabu,almasi na vito vingine vya thamani pamoja na mamilioni ya fedha taslimu kinyume na sheria. Hata mkewe Leila Trabelsi aliejulikana kwa maisha yake ya fahari, amepewa kifungo cha miaka 35. Jaji Touhami Hafi aliesoma hukumu ya adhabu hiyo mahakamani katika mji mkuu Tunis alisema kuwa Ben Ali na mkewe watapaswa kulipa faini ya dola milioni 65.6 vile vile.

Ben Ali adai mashtaka ni njama ya kisiasa

FILE - In this Oct.28 2010 file photo, Leila Ben Ali, wife of Tunisian President Zine El Abidine Ben Ali, attends the opening session of the 3rd Congress of the Arab Women's Organisation in Tunis. Tunisians cheering a new era after the end of President Zine El Abidine Ben Ali's iron-fisted rule are especially overjoyed at the prospect of life with out his wife and her family - widely despised as the ultimate symbol of corruption and excess. (Foto:Hassene Dridi, File/AP/dapd)
Leila Trabelsi, mkewe Ben AliPicha: dapd

Kwa mujibu wa ripota mmoja wa shirika la habari la Reuters aliekuwepo mahakamani, hukumu juu ya mashtaka mengine ya kudhibiti madawa ya kulevya na silaha itatolewa Juni 30. Katika taarifa iliyotolewa mapema hiyo jana na mawakili wanaomtetea Ben Ali, rais huyo wa zamani alisema kwamba silaha anazotuhumiwa kudhibiti kinyume na sheria, zilikuwa zawadi kutoka viongozi wa kimataifa; na vito vya thamani, ni zawadi zilizotolewa na wanadiplomasia wa kigeni kwa mke wake Leila. Amesema, fedha taslimu na madawa, yalipelekwa nyumbani kwake na katika makao rasmi ya rais, baada ya yeye kuondoka nchini humo. Amesema, hiyo ilikuwa njama dhidi yake. Ben Ali, amekanusha mashtaka yote dhidi yake. Akaongezea kuwa yeye ni mhanga wa njama ya kisiasa na kwamba alifanyiwa ujanja kuondoka Tunisia.

Kesi ya Ben Ali imefuatilizwa kwa makini Misri

Ben Ali , mkewe na watoto wao walikimbilia Saudi Arabia Januari 14 mwaka huu, baada ya kushinikzwa na maandamano makubwa ya kupinga utawala wake wa miaka 23 nchini Tunisia. Wakati wa utawala huo, Ben Ali, familia yake na ya mkewe zilijirundikia mali; na wale waliothubutu kumpinga, walikamatwa na vikosi vya usalama. Mapinduzi ya Tunisia yaliwasisimua mamilioni ya watu katika ulimwengu wa Kiarabu, wakiwa na matatizo yale yale ya ukosefu mkubwa wa ajira, ughali wa maisha na serikali za ukandamizaji. Kesi ya Ben Ali imefuatilizwa kwa makini nchini Misri, ambako rais wa zamani wa nchi hiyo Hosni Mubarak, anatazamiwa pia kupandishwa kizimbani kwa mashtaka ya mauaji ya waandamanaji.

epa02779510 (FILE) A file photograph dated 13 December shows the former Tunisian President Zine El Abidine Ben Ali at the airport Tunis-Carthage in Tunis, Tunisia. According to media reports on 13 June 2011, Tunisia's ousted ex-leader Zine el-Abidine Ben Ali and his wife Leila will be trialed in absentia on 20 June 2011. Ben Ali fled to Saudi Arabia after he was toppled by mass protests on 14 January after 23 years in power. EPA/STR +++(c) dpa - Bildfunk+++ usage Germany only, Verwendung nur in Deutschland
Rais wa zamani wa Tunisia, Zine al-Abidine Ben AliPicha: picture-alliance/dpa

Mwandishi: Martin,Prema/rtre

Mhariri:Abdul-Rahman