1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Benazir Bhutto azikwa karibu na kaburi la babake

28 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/ChZS

RAWALPINDI:

Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan-Benazir Bhutto,amezikwa karibu na wanakozikwa watu wa familia ya Bhutto katika mkoa wa Sindhi.

Amezikwa karibu na alipozikwa waziri mkuu wa kwanza wa nchi hiyo Zulfika Ali Bhutto.

Mamia kwa maelfu ya waombolezaji walikusanyika ili kuhudhuria mazishi hayo.Mazishi haya yametokea siku moja tu baada yakuuawa kwa kupigwa risasi alipokuwa anatoka kuhutubia mkutano wa mjini Rawalpindi.

Kuuliwa kwake kumezusha fujo na ghasia katika nchi hiyo.

Maafisa wa serikali wanasema watu wasiopungua 19 wameuawa katika ghasia hizo.

Vikosi vya usalama katika mkoa wa Sindhi, vimeamuriwa kumpiga risasi yeyote atakaekuwa anafanya fujo. Licha ya kifo cha Bi Bhutto,waziri mkuu wa sasa wa Mohammadmian Soomro amesema kuwa serikali haina mipango yoyote ya kuahi-rishwa kwa uchaguzi ambao umepangwa kufanyika mwezi ujao.

Kwa mda huohuo mauaji ya Bi Bhutto , yanaendelea kulaaniwa na jamii ya kimataifa.Kufuatia kikao maalum cha baraza la usalama la umoja wa Mataifa,Katibu mkuu wa Ban Ki-moon ameyaelezea mauaji hayo kama tukio la kigaidi. Kansela wa Ujeruamni -Angela Merkel -amekielezea kisa hicho kama tukio la kigaidi la kiuoga. Nae waziri wa mashauri ya kigeni wa Ujerumani- Frank –Walter Steinmeier amesema kuwa ni pigo kubwa kwa juhudi za kurejesha demokrasia nchini Pakistan.