1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Benedikt wa 16 aomba dua ya amani

Oumilkher Hamidou7 Desemba 2008

Kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni awaomba waumini wawaombee wahanga wa mashambulio ya Jos na Mumbai

https://p.dw.com/p/G6JJ

Vatican City:


Kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni Benedikt wa 16 ametoa mwito wa kuwaombea duwa wahanga wa mashambulio ya India na wa matumizi ya nguvu nchini Nigeria.Akiwahutubia waumini waliokusanyika katika uwanja wa Saint Peter mjini Vatican kiongozi huyo wa kanisa katoliki ulimwenguni ameyalaani mashambulio hayo na kuyataja kua ni ya kikatili na yasiyokua na maana.Ametoa mwito watu wawe na imani na upendo kuweza kujenga jamii inayostahiki mbele ya Mungu na walimwengu.