1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Uchumi

Benki Kuu ya Ulaya kuzindua sarafu ya dijitali

Sylvia Mwehozi
19 Oktoba 2023

Baraza la uongozi la ECB limesema kwamba litaanza awamu ya maandalizi ya miaka miwili kwa ajili ya uzinduzi wa sarafu ya kidijitali mnamo Novemba mosi.

https://p.dw.com/p/4XjJu
Yuro
Sarafu ya yuroPicha: FabrikaSimf/IMAGO/Pond5 Images

Benki Kuu ya Ulaya ECB imepiga hatua kuelekea kuzindua toleo la sarafu ya kidijitali ya Yuro. Baraza la uongozi la ECB limesema kwamba litaanza awamu ya maandalizi ya miaka miwili kwa ajili ya uzinduzi wa sarafu ya kidijitali mnamo Novemba mosi ili kukamilisha sheria na kuchagua washirika wa sekta binafsi. EU kuchukuwa hatua kuelekea euro ya kidijitali

Awamu ya maandalizi itajumuisha hatua ya majaribio, kutokana na kwamba tathmini juu ya manufaa au hatari zinazohusiana na sarafu ya kidijitali bado hazijawekwa wazi.

ECB ilishikilia kuwa uamuzi wa mwisho wa kuzindua sarafu ya kidijitali bado haujafafikiwa. Sarafu ya kidijitali ya yuro itakuwa ni pesa ya kielektroniki itakayotumiwa na kila mtu katika eneo linalotumia sarafu ya yuro.

Zaidi ya benki kuu 100 duniani kote, ikiwa ni pamoja na China na Japan, zinajitayarisha kuanzisha sarafu zake za kidijitali kadri malipo ya kielektroniki yanavyoongezeka.