1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Benzema apata matumaini ya Euro 2016

11 Machi 2016

Habari nzuri kwa mshambuliaji wa Ufaransa na Real Madrid Karim Benzema maana sasa yuko huru kucheza katika dimba la kombe la mataifa ya Ulaya Euro 2016

https://p.dw.com/p/1IBt0
Französischer Fußballspieler Karim Benzema
Picha: picture-alliance/dpa/A. Taherkenareh

Hii ni baada ya vizuizi vya kisheria vilivyowekwa dhidi yake kuhusiana na madai ya kuhusika kwake katika sakata la usaliti wa kanda ya ngono kuondolewa jana Ijumaa. Hayo ni kwa mujibu wa wakili mchezaji huyo Olivier Combe. "nataka tu kusema kuwa mahakama ya rufaa ya Versailles [Ver-saa-ye] imeshikilia uamuzi wa hakimu anayechunguza kesi hiyo, hivyo kumruhusu Benzema kukutana na Mathieu Valbuena. Sina taarifa nyingine ya kutoa, huu ni uamuzi wa kuridhisha sana.

Chini ya vikwazo hivyo, Benzema hakuruhusiwa kuwasiliana au kuwa karibu na mchezaji mwenzake wa Ufaransa Mathieu Valbuena ambaye alilengwa katika jaribio hilo la usaliti.

Lakini mahakama ya rufaa imeushikilia uamuzi wa hakimu anayechunguza kesi hiyo wa kuondoa vikwazo, hali inayomruhusu Benzema kujumuishwa katika kikosi cha taifa pamoja na Valbuena, ikiwa wachezaji hao wawili watachaguliwa kushiriki katika dimba hilo litakaloandaliwa Ufaransa.

Kocha wa Ufaransa Didier Deschamps alimwondoa Benzema mwenye umri wa miaka 28 katika timu ya taifa baada ya kuwekwa chini ya uchunguzi rasmi kuhusiana na suala hilo mwezi Novemba. Licha ya uamuzi wa jana wa mahakama ya rufaa Benzema angali chini ya uchunguzi.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/AP
Mhariri: Gakuba Daniel