1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Angela Merkel kutembelea mashariki ya kati

4 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCdP

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel anatarajiwa kufanya ziara ya mashariki ya kati mwezi ujayo, ikiwa ni sehemu ya majukumu yake kama rais wa umoja wa ulaya kuimarisha amani katika eneo hilo.

Kansela Merkel atazitembelea Misri, Saudi Arabia, Falme za Kiarabu na Kuwait.Msemaji wa ofisi ya Kansela Merkel amesema kuwa ziara hiyo inatarajiwa kuweka msukumo mpya katika ufufuaji wa juhudi za pande nne kutafuta amani ya mashariki ya kati.Pande hizo nne ni umoja wa ulaya, umoja wa mataifa, Urusi na Marekani.

Wakati huo huo Kansela Angela Merkel leo anaelekea Washington ambako anatarajiwa kuwa na mazungumzo na rais George Bush yanayotarajiwa kujikita katika uhusiano wa kibiashara kati ya umoja wa ulaya na Marekani.