1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Chile yavutia vitega uchumi vya Ujerumani.

20 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD0w

Rais wa Chile Michelle Bachelet anaendelea na ziara yake nchini Ujerumani. Jana Alhamis alikuwa na mazungumzo na kansela wa Ujerumani Angela Merkel pamoja na wanasiasa wengine.

Merkel ametoa uhakikisho kuwa Ujerumani itaunga mkono juhudi za Bachelet kuleta usawa zaidi na haki kwa raia nchini Chile.

Bachelet amesema ziara yake ilikuwa na lengo la kuwavutia wawekezaji vitega uchumi kutoka Ujerumani.