1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Hakukuwepo magereza ya siri ya CIA Ujerumani

7 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD5S

Ujerumani imekanusha madai yaliyotolewa na kundi la kutetea haki za binaadamu la Uingereza kwamba Shirika la Ujasusi la Marekani CIA yumkini likawa limetumia kambi ya anga ya Marekani nchini Ujerumani kushikilia watuhumiwa wakiwemo wanachama wa kundi la Al Qaeda kabla ya kuhamishiwa Guantanamo.

Msemaji wa serikali ya Ujerumani Thomas Steg amesema kulikuwa hakuna siri katika vituo vya magereza vya Marekani nchini Ujerumani.Kundi hilo la haki za binaadamu la Reprieve ambalo linawakilisha mahabusu kadhaa wa Guantanamo kambi ya magereza ya Marekani ilioko nchini Cuba limesema lina ushahidi kutoka kwa mahabusu watatu na kwamba kila mmoja alikuwa anajuwa juu ya watuhumiwa waliokuwa wakishikiliwa au kuhamishwa kupitia makambi ya Marekani nchini Ujerumani.

Mwezi uliopita Rais George W Bush wa Marekani amekiri kwamba CIA iliwasaiili madarzeni ya watuhumiwa katika vituo vya siri nchi za nje ambavyo hakusema wapi.

Hapo mwezi wa Juni mchunguzi wa Baraza la Ulaya Dick Marty amedai kwamba kambi ya Marekani huko Ramstein magharibi mwa Ujerumani ilikuwa ni kitovu cha safari za ndege za siri.