1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Idadi ya wenye ajira yaongezeka

27 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBME

Idadi ya watu wenye ajira nchini Ujerumani imeongezeka na kufikia kiwango cha juu kuwahi kushuhudiwa baada ya kuungana tena kwa Ujerumani na kuwa watu zaidi ya milioni 39.7.

Takwimu za hivi karibuni kutoka Ofisi ya Takwimu ya serikali ya shirikisho zimeonyesha kwamba ajira imeongezeka kwa watu 19,000 hapo mwezi wa Augusti ikiwa ni ongezeko kwa miezi 19 mfululizo.Kutolewa kwa data hizo za ajira kunakuja wakati Ofisi ya Ajira ya serikali ya Ujerumani ikiandaa kutangaza takwimu za ukosefu wa ajiara kwa mwezi wa Septemba.

Wachambuzi wa mambo wanategemea kiwango cha ukosefu wa ajira cha asilimia 8.9 ikiwa ni kiwango cha chini kabisa tokea mwaka 1993 na chini kutoka asilimia 9 hapo mwezi wa Augusti.