1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Köhler na Merkel wamempongeza Ban Ki Moon

14 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD2q

Rais Horst Köhler na Kansela Angela Merkel wa Ujerumani wamempongeza Ban Ki Moon aliechaguliwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa.Köhler amemtakia nguvu na uvumilivu kuungoza Umoja wa Mataifa kwa mafanikio katika siku zijazo. Utaratibu wa mageuzi ulioanzishwa na Katibu Mkuu Kofi Annan lazima uendelee.Merkel amemuhakikishia Ban kuwa serikali ya Ujerumani itamuunga mkono. Siku ya Ijumaa,Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilimchagua waziri wa mambo ya kigeni wa Korea ya Kusini kuwa Katibu Mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa.Ban,atamrithi Kofi Annan tarehe mosi Januari.Annan,mwezi wa Desemba anakamilisha awamu yake ya pili kama Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na hivyo hawezi kugombea tena wadhifa huo.