1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Kansela Merkel atetea tume ya kulinda amani Afghanistan

16 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBPR

Kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel amesema tume ya kulinda amani nchini Afghanistan inahitajika ili kupambana na ugadi wa kimataifa.

Bi Merkel ameyasema hayo baada ya maelfu ya waandamanaji kuandamana kwenye barabara za mji mkuu Berlin hapo jana wakitaka Ujerumani iwaondoe wanajeshi wanaolinda amani nchini Afghanistan.

Katika taarifa yake ya kila wiki kansela Merkel amesisitiza kwamba kuwasaidia Waafghanistan kuijenga nchi yao ndio njia pekee ya kuizia nchi hiyo kutumiwa kama uwanja wa mafunzo kwa magaidi.

Takriban wanajeshi 3,000 wa Ujerumani wako katika eneo la kaskazini mwa Afghnistan kama sehemu ya kikosi cha ISAF cha jumuiya ya kujihami ya kambi ya magharibi, NATO.

Katika mkutano wake chama cha Kijani cha hapa Ujerumani kimepinga mswada wa serikali ya kansela Merkel unaotaka wabunge wapige kura kuunga mkono kurefushwa muda kwa wanajeshi wa Ujerumani waendelee kubakia nchini Afghanistan.

Chama cha Kijani pia kinapinga ndege za Ujerumani zisitumike kupiga picha kuchunguza miendendo ya waasi wa Taliban nchini Afghanistan.