1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Kansela wa zamani amemtetea waziri Steinmeier

2 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCVt

Kansela wa zamani wa Ujerumani,Gerhard Schroeder amemtetea waziri wa kigeni Frank-Walter Steinmeier dhidi ya madai kuwa alisaidia kuchelewesha kuachiliwa huru,Mturuki aliezaliwa Ujerumani Murat Kurnaz,kutoka jela ya kijeshi ya Marekani,Guantanamo Bay.Steinmeier anaesisitiza kwamba hakuwa na habari iliyohusika na “pendekezo rasmi“ anatazamiwa kutoa ushahidi wake tarehe 8 mwezi Machi,mbele ya kamati ya bunge inayofanya uchunguzi.Steinmeier,anatuhumiwa kuwa alipuuza pendekezo la Marekani la kutaka kumuachia huru Kurnaz kutoka jela ya Guantanamo Bay hapo mwaka 2002.Kurnaz alikamatwa mwaka 2001 nchini Pakistan akishukiwa kuwa ni gaidi na aliachiliwa huru mwaka jana,bila ya kufikishwa mahakamani.