1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Kiongozi wa kampuni la Siemens kujiuzulu.

26 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC6y

Mtendaji mkuu wa kampuni kubwa la uhandisi nchini Ujerumani la Siemens amesema kuwa atajiuzulu mwishoni mwa Septemba.

Wakati huo ndio mkataba wa sasa wa kiongozi huyo Klaus Kleinfeld utakapomalizika.

Kleinfeld ameiambia bodi ya uendeshaji ya kampuni hilo kuwa amefikia uamuzi huo baada ya kufahamu kuwa baadhi ya wajumbe wa bodi wanapingana na hatua ya kutaka kurefusha mkataba wake.

Kleinfeld ameshutumiwa kwa kushindwa kufanya lolite kwa haraka kulishughulikia suala la rushwa katika kampuni hilo la Siemens.

Madai hayo ni pamoja na kuwa ma milioni ya Euro yaliyotolewa kama hongo yamelipwa ili kupata mikataba nje ya nchi.

Uchunguzi uliofanywa ndani ya kampuni hilo la Siemens umemuweka mbali Kleinfeld na tuhuma hizo.