1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Maafikiano kuhusu wahamiaji wasio na vibali

15 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCsi

Serikali ya muungano mkuu nchini Ujerumani imeafikiana kuhusu haki ya kubakia Ujerumani kwa maelfu ya wahamiaji walio nchini hivi sasa bila ya vibali vya kuishi.Kuambatana na maafikiano hayo,wale wanaoweza kujitegemea na kutazama familia zao bila ya msaada wa serikali wataruhusiwa kuendelea kuishi Ujerumani.Familia zenye watoto zitakuwa na haki hiyo baada ya kuwepo nchini kwa muda wa miaka sita na wajane baada ya miaka minane.Hivi sasa,kiasi ya wahamiaji 190,000 wanavumiliwa Ujerumani bila ya vibali vya kubakia nchini.Maafikiano hayo sasa yanahitaji kuidhinishwa na serikali za majimbo 16.Wakati huo huo katika vita vya kupambana na tatizo la uhamiaji usio halali,waziri wa masuala ya ndani wa Ujerumani,Wolfgang Schäuble ametoa mwito wa kuchukuliwa hatua za kuwarejesha makwao wahamiaji wanaoingia kinyume cha sheria.