1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Mabomu ya mtawanyo yapigwe marufuku duniani

20 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD16

Serikali ya Ujerumani imesema,suala la kupunguza nguvu za silaha litakuwa kipaumbele kwenye mkutano wa kilele wa madola yalio tajiri kiviwanda duniani-G8,pale Ujerumani itakaposhika wadhifa wa kuongoza mkutano huo.Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani,Frank-Walter Steinmeier amesema atautumia mkutano huo kuhimiza kuwa kutakuwepo udhibiti mkali zaidi kuhusu teknolojia ya kinuklia.Mabomu ya mtawanyo vile vile yapigwe marufuku kote duniani.Wakati huo huo shirika linalotetea haki za binadamu,”Human Rights Watch” limewatuhumu wanamgambo wa Hezbollah kuwa walirusha makombora yenye mabomu ya mtawanyo katika ardhi ya Israel wakati wa vita vya hivi karibuni.Idadi hiyo lakini ni robo ya yale yaliorushwa na Israel nchini Lebanon.Kwa makisio ya ya Umoja wa Mataifa,Israel ilirusha hadi mabomu milioni nne ya mtawanyo nchini Lebanon. Inakadiriwa kuwa kama mabomu milioni moja hayakuripuka na yanaendelea kuwatia raia hatarini.Tangu vita vya Israel na Hezbollah kumalizika Agosti 14,mabomu hayo yameuwa Walebanon 20 na wengine 120 wamejeruhiwa-wengi wao wakiwa ni watoto.