1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Mada kuu ni dhima za kijamii za makampuni makubwa

4 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCMR

Rais Horst Köhler wa Ujerumani yupo njiani kuelekea Paraguay akianza ziara yake rasmi ya kwanza barani Amerika ya Kusini.Hii ni mara ya kwanza kabisa kwa rais wa Kijerumani kuitembelea rasmi Paraguay.Wakati wa ziara hii ya siku 12, Köhler atazitembelea Brazil na Colombia vile vile.Mada kuu ya ziara hii ni kushughulikia dhima za kijamii za makampuni kuhusika na ugawaji wa mapato usio na usawa,ikizingatiwa hali iliopo hivi sasa katika nchi za Amerika ya Kusini.Rais Köhler amefuatana na tume ya wanauchumi.