1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Mageuzi katika idara ya upelelezi BND

27 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7CF

Idara ya upelelezi wa nje ya Ujerumani-BND itafanyiwa mageuzi.Ifikapo mwaka 2009,idara hiyo yenye wafanyakazi 6,000 itakuwa na mfumo mpya kabisa.Badiliko moja kuu ni kuondoshwa kwa utaratibu unaotenganisha huduma za idara inayokusanya habari na ile inayochambua habari hizo.

Siku hizi za karibuni,idara hiyo ya upelelezi imezidi kushinikizwa kufanya mageuzi baada ya kutokea kashfa mbali mbali.Mojawapo ni ripoti kwamba maafisa wa BND wamewapeleleza waandishi wa habari nchini Ujerumani.