1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Maonyesho ya kimataifa ya utalii yaendelea

9 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCKy

Maonyesho ya kimataifa ya utalii yanaendelea mjini Berlin Ujerumani. Kwa mujibu wa kiongozi wa shirika la utalii la Umoja wa Mataifa, Francesco Frangialli, faida ya kifedha kutokana na utalii inaendelea kuimarika huku watalii wakipuuza vita na mizozo na kuendelea na safari zao.

Akizungumza katika maonyesho ya ITB mjini Berlin, kiongozi huyo amebashiri kuwa utalii utaongezeka kwa asilimia 4 katika miaka ijayo akisisitiza mataifa maskini ndiyo yatakayofaidi zaidi kutokana na utalii.