1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Mashahidi wahojiwa kuhusu Murat Kurnaz

1 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCW7

Kamati ya bunge la Ujerumani,inayochunguza mkasa wa kutiwa jela ya Guantanamo Bay,Mturuki aliezaliwa Ujerumani,itawahoji mashahidi wakuu 3 ambao ni mawakala katika idara ya upelelezi ya Ujerumani-BND.Wote watatu,walimhoji Murat Kurnaz wakati alipokuwa katika jela ya kijeshi ya Marekani,Guantanamo Bay.Kamati hiyo inayokutana mjini Berlin kwa faragha,inatazamiwa pia kupanga tarehe ya kupata ushahidi kutoka waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier. Kurnaz alikamatwa mwaka 2001 nchini Pakistan akishukiwa kuwa ni gaidi na aliachiliwa huru mwaka jana bila ya kufikishwa mahakamani.Kurnaz na wakili wake,wameituhumu wizara ya kigeni ya ujerumani,kuwa ilipuuza pendekezo la Marekani la kutaka kumuachilia huru hapo mwaka 2002.