1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Mbunge ashtakiwa kwa ulaghai

5 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCdI

Mbunge wa bunge la Ujerumani anakabiliwa na mashtaka kuhusiana na kashfa ya rushwa katika kampuni kubwa kabisa ya kutengeneza magari barani Ulaya ya Volkswagen.

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya waendesha mashtaka mjini Braunschweig imesema Hans- Jürgen Uhl amefunguliwa mashtaka mawili ya kushirika kwenye ulaghai na kusema uongo wakati wa kiapo.Wakati wa kutokea kwa uhalifu huo unaodaiwa mwanasiasa huyo wa chama cha Social Demokrat alikuwa ni mjumbe mwandamizi wa baraza la kazi la Volkswagen.

Kashfa hiyo imetuwama kwenye madai kwamba wawakilishi wa wafanyakazi na wajumbe wa baraza la kazi walipokea bakshishi na marupurupu yasio halali ili waidhinishe hatua za kujiunda upya kwa kampuni hiyo.

Uhl anakuwa mtu wa pili kushtakiwa mkurugenzi wa zamani wa kitengo cha wafanyakazi cha kampuni ya Volkswagen Peter Hartz anatarajiwa kufikishwa mahkamani baadae mwezi huu.