1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Meneja mkuu wa Volkswagen akamatwa katika kashfa ya rushwa

22 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCqS

Kiongozi wa zamani wa kampuni ya magari ya Volkswagen amekamatwa katika uchunguzi wa kile kilichotajwa kashfa ya rushwa kwenye kampuni kubwa kabisa inayotengeneza magari barani Ulaya. Klaus Volkert amekamatwa wiki moja baada ya kushtakiwa kwa makosa 44 ya udanganyifu. Uchunguzi unafanyika juu ya madai kwamba mameneja wa kampuni na wajumbe wa baraza tendaji walijipangia marupurupu kupita kiasi yanayolipwa na kampuni.

Upande wa kibiashara, Volkswagen imetangaza uwezekano mkubwa kukifunga kiwanda chake kilichoko karibu na mji mkuu wa Ubelgiji Brussels na kukirudisha nchini Ujerumani.

Kiongozi wa chama cha wafanyakazi amesema hatua hiyo itapelekea watu takriban 4,000 kupoteza kazi.