1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Merkel aipongeza Marekani

8 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCcQ

Kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel ameikaribisha hatua ya Marekani kujihusisha tena katika kuumaliza mzozo wa Mashariki ya Kati. Akizungumza kwenye kituo cha runinga cha ZDF hapa nchini, kansela Merkel ameongeza kusema kwamba mazungumzo ya hivi karibuni kati ya viongozi wa Palestina na Israel yanatoa mwanya wa kuziendeleza juhudi za kutafuta amani kati ya waisraeli na wapalestina.

Kansela Merkel anataka pande nne zinazioudhamini mpango wa amani ya mashariki ya kati, zikiwemo Umoja wa Ulaya, Urusi, Umoja wa Mataifa na Marekani, ziyafufue na kuyaongoza mazungumzo ya amani ya mashariki ya kati.