1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Merkel amaliza ziara yake Uturuki.

7 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD5G

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amekamilisha ziara yake ya siku mbili nchini Uturuki ambako amelenga zaidi katika mahusiano ya kibiashara lakini amesita kuiunga mkono nchi hiyo katika juhudi zake za kujiunga na umoja wa Ulaya .

Maguezi yaliyofanywa na Uturuki hadi sasa , amesema , yamekwisha imarisha uchumi wa nchi hiyo.

Merkel ambaye chama chake cha kihafidhina nchini Ujerumani kinataka ushirika wa upendeleo kwa Uturuki, amesema umoja huo na Uturuki zinapaswa kujiepusha na vikwazo vingine katika mzozo wao juu ya mahusiano ya kibiashara na Cyprus.

Waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesisitiza kuwa umoja wa Ulaya uondoe vikwazo vyake dhidi ya eneo la kaskazini la kisiwa cha Cyprus linalokaliwa na Waturuki.

Uturuki inakataa kufungua bandari zake na viwanja vya ndege kwa Cyprus hadi pale umoja wa Ulaya utakapofanya hivyo. Merkel na Erdogan baadaye walikutana na viongozi wa dini ya Kiislamu na Wakristo wa madhehebu ya Orthodox nchini humo.