1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Merkel amesifu mradi wa Blair kuhusu mazingira

14 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCJB

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani na Kamishna wa Mazingira wa Umoja wa Ulaya,Stavros Dimas wamefurahia hatua iliyochukuliwa na Uingereza kuwa nchi ya kwanza kupendekeza sheria itakayoweka viwango vya utoaji wa gesi ya kaboni dayoksaidi inayochafua mazingira.Kansela Merkel amesema hatua inayochukuliwa na Uingereza ni barabara.Wakati huo huo Dimas amesema,sheria inayotazamiwa kupitishwa na Uingereza ni hatua ya ushujaa inayotoa mfano mzuri kwa wanachama wengine wa Umoja wa Ulaya.Mswada huo wa sheria kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa,unapendekeza kupunguza utoaji wa gesi ya kaboni dayoksaidi kwa asilimia 60 ifikapo mwaka 2050.Hatua hiyo imechukuliwa na Uingereza siku chache tu baada ya viongozi wa Umoja wa Ulaya kukubaliana kupunguza utoaji wa gesi hiyo kwa asilimia 20 ifikapo mwaka 2020.