1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Merkel amuunga mkono Steinmeir

23 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCYk

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani na washirika wenzake kwenye serikali ya mseto wa chama cha Social Demokrat wamemuunga mkono Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmeir juu ya dhima yake wakati wa kushikiliwa kwa Mturuki mzalia wa Ujerumani katika kambi ya Guantanamo nchini Cuba.

Murat Kurnaz aliachiliwa huru na Marekani mwezi wa Augusti mwaka jana baada ya kushikiliwa kwa zaidi ya miaka minne bila ya kufunguliwa mashtaka.Msemaji wa serikali ya Ujerumani amesema Merkel anamwamini Steinmeir na amewataka wakosoaji wake wasubiri uchunguzi unaofanywa na kamati ya bunge.

Vyama vya upinzani vinataka Steinmeir ambaye alikuwa waziri wa nchi katika ofisi ya Kansela katika serikali iliopita ya Ujerumani iliokuwa ikiongozwa na chama cha Social Demokrat kujibu madai kwamba Ujerumani ilizuwiya kuachiliwa kwa Kurnaz hapo mwaka 2002.

Wiki iliopita Kurnaz aliambia kamati ya bunge la Ujerumani kwamba aliteswa na Wamarekani wakati akiwa mahabusu huko Guantanamo.