1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Merkel atarajiwa kuwasili Marekani leo

4 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCdV

Kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel anatarajiwa kuwasili leo mjini Washington Marekani kukutana na rais wa nchi hiyo, George W Bush katika juhudi za kuboresha ushirikiano baina ya Marekani na Umoja wa Ulaya.

Wakati haya yakiarifiwa, kansela Merkel anatarajiwa pia kusafiri kwenda mashariki ya kati wiki ijayo ikiwa ni sehemu ya majukumu ya nchi yake kama kiongozi wa Umoja wa Ulaya kuupiga jeki mpango wa amani ya mashariki ya kati.

Bi Merkel atazitembelea Misri, Saudi Arabia, Umoja wa falme za kiarabu na Kuwait. Msemaji wake amesema ziara ya Merkel huenda ikaupa mwelekeo mpya mpango wa amani ya mashariki ya kati unaodhaminia na Umoja wa Ulaya, Urusi, Umoja wa Mataifa na Marekani.