1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Merkel ziarani Uturuki.

5 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD60

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel anakwenda nchini Uturuki leo kwa ziara ya siku mbili, ambapo anatarajiwa kusisitiza dai la umoja wa Ulaya la kuondolewa kwa vikwazo vyake vya biashara dhidi ya Cyprus.

Atakapowasili mjini Ankara , Merkel atatoa heshima zake katika kaburi la Kemal Ataturk, muasisi wa Uturuki ya sasa , na kupata chakula cha jioni na waziri mkuu Recep Tayyip Erdogan wakati akifuturu kwa mfungo wa Ramadhan.

Maafisa wa Ujerumani wamesema kuwa Merkel anatarajiwa pia kuzusha masuala nyeti kama vile kukataa kwa Uturuki kuiruhusu Cyprus kutumia bandari zake na viwanja vya ndege , licha ya ahadi za Uturuki za kuidhinisha umoja wa forodha na umoja wa Ulaya.