1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Mfungwa wa zamani wa Guantanamo, Murat Kunaz aeleza hali ya Marekani kukiuka haki za binadamu nchini Afghanistan.

18 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCZu

Mfungwa wa zamani wa gereza la Guantanamo, Murat Kurnaz ameieleza tume ya uchunguzi ya bunge la Ujerumani kuhusu vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu vinavyofanywa katika kambi Marekani nchini Afghanistan.

Murat Kurnaz, mturuki ambaye ni mzaliwa wa Ujerumani aliwaambia wabunge kwamba alikuwa akifungwa kwa minyororo na kuning`inizwa kwa siku kadhaa hadi madaktari walipokuja kumchunguza iwapo mwili wake ungestahamili mateso hayo.

Murat Kurnaz aliyarejea madai yake kwamba askari wawili wa Kijerumani walimpiga wakati akizuiliwa nchini Afghanistan.

Kurnaz alikamatwa mwaka 2002 nchini Pakistan na kupelekwa Guantanamo Bay kisha akaachiwa huru bila kushtakiwa mwaka uliopita.