1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Mkutano kuhusu Afghanistan wafanyika leo

29 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCWh

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Afghanistan, Daddfar Spanta, yumo mjini Berlin kwa mazungumzo na maofisa wa Umoja wa Ulaya kuhusu juhudi za kuijenga upya Afghanistan.

Mkutano huo unafanyika wakati kukiwa na hofu ya wanamgambo wa Taliban kufanya mashambulio kadhaa nchini Afghanistan.

Umoja wa Ulaya umeahidi kutoa euro milioni 600 kwa ujenzi wa Afghanistan katika kipindi cha miaka minne ijayo. Lakini kwenye mkutano wa shirika la NATO uliofanyika wiki iliyopita mjini Brussels Ubelgiji, Marekani iliwatolea mwito washirika wake barani Ulaya waongeze misaada yao na idadi ya wanajeshi nchini Afghanistan.