1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN ; Msimamo wa kundi la pande nne wasisitizwa

23 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCPa

Rais Mahmoud Abbas wa Palestina ameyataka mataifa makubwa duaniani kuondowa kususiwa kwa msaada wa kiuchumi dhidi ya serikali ya Palestina kulikowekwa baada ya kundi la Hamas kuingia madarakani hapo mwaka jana.

Kufuatia mkutano wake na waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmeir mjini Berlin Abbas amesema kwamba serikali mpya ya umoja wa kitaifa itajifunga kuepusha umwagaji damu.Steinmeir amesisitiza msimamo wa kundi la pande nne linaloshughulikia amani ya Mashariki ya Kati.

Katika mkutano huo katika mji mkuu wa Ujerumani Berlin hapo Jumatano kundi hilo la pande nne linalojumuisha Marekani,Urusi, Umoja wa Ulaya na Umoja wa Mataifa limekubaliana kuahirisha kutowa msimamo wao hadi hapo serikali hiyo mpya ya Wapalestina itakapokuwa imeundwa.

Kundi hilo la pande nne linadai serikali hiyo ikanushe matumizi ya nguvu na itambuwe haki ya kuwepo kwa taifa la Israel jambo ambalo daima limekuwa likikataliwa na Hamas.