1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Pelosi amsifu Merkel kwa ujasiri.

30 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBwo

Spika wa baraza la wawakilishi nchini Marekani , Nancy Pelosi aliyeko ziarani mjini Berlin, amemsifu kansela Angela Merkel kwa uongozi wake wa kijasiri, katika juhudi zake za kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Pelosi ameahidi uungaji mkono wa baraza la Congress , ambalo linadhibitiwa na chama cha Democratic , katika kupata makubaliano ya kimataifa ili kuzuwia hali ya ujoto isiongezeka.

Maelezo hayo ni kinyume na rais George W. Bush , ambaye kwa muda wa miaka mitano iliyopita ameyapa mgongo makubaliano ya Kyoto.

Mshauri wake wa masuala ya hali ya hewa James Connaughton, ambaye pia anafanya ziara mjini Berlin, amesema kuwa Marekani haiamini kuwa mataifa tajiri yenye viwanda G8 yatakubaliana na malengo kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa ya kansela Merkel katika mkutano wa wiki ijayo nchini Ujerumani.

Mataifa mengine , amesema , hayako tayari kuidhinisha malengo ya umoja wa Ulaya ya kupunguza ujoto kwa kiwango cha nyuzi joto mbili ikilinganishwa na wakati kabla ya enzi za viwanda.