1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Pelosi azunguzia mazingira.

29 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBx8

Spika wa baraza la wawakilishi nchini Marekani Nancy Pelosi, ambaye anapingana na rais wa Marekani George W. Bush kuhusiana na masuala ya mazingira, amekutana na mawaziri wa serikali ya Ujerumani mjini Berlin.

Waziri wa mazingira wa serikali ya Ujerumani , Siegmar Gabriel , ameeleza kusikitishwa kwake kwa Marekani kukataa kuchukua hatua madhubuti dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Pelosi , kutoka chama cha Democratic , amesema kuwa ataendelea kulijadili suala hilo na utawala wa rais Bush. Anatarajiwa kukutana na kansela wa Ujerumani Angela Merkel baadaye leo.