1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Rais Chirac akutana na kansela Merkel

23 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCPS

Rais wa Ufaransa Jacques Chirac na kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel wanakutana leo nje ya mji wa Berlin katika mkutano wa kilele ambao hufanyika baina yao mara kwa mara.

Mkutano huo utazungumzia kwa kina mpango wa kuifanyia mageuzi kampuni ya ndege ya Airbus. Maelfu ya nafasi za ajira zinatarajiwa kupotea nchini Ujerumani na Ufaransa huku kampuni ya EADS ikijiandaa kutekeleza mpango wa kupunguza matumizi kwa kiasi cha euro milioni tano katika kipindi cha miaka mitatu ijayo. Maafisa wa Ujerumani na Ufaransa wamekuwa wakizozana juu ya wapi nafasi za ajira zipunguzwe.

Kampuni ya EADS imesema itatoa maelezo ya kina kuhusu mpango wa kupunguza matumizi kabla kutoa takwimu za mapato yake ya kila mwaka mnamo tarehe 9 mwezi ujao.