1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Rais Köhler anasema mwaka 2006 ulikuwa mzuri

26 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCg3

Rais Horst Köhler wa Ujerumani akitoa hotuba yake ya kila mwaka ya kusheherekea X’masi amewataka wananchi wa Ujerumani kuuangalia mwaka mpya unaokuja kwa matumaini.

Köhler ameuelezea mwaka 2006 kuwa ni mwaka ulioadhimishwa kwa mabadiliko ndani ya Ujerumani kwenyewe na kwa namna nchi hii inavyoangaliwa nchi za nje.Amesema jambo hilo lilijidhihirisha wazi hususan wakati wa michuano ya kandanda ya Kombe la Dunia wakati wa kipindi cha kiangazi kilichopita cha mwaka huu.

Rais pia alikuwa na matumaini juu ya hali ya uchumi kwa kudokeza kupunguka kwa kiwango cha ukosefu wa ajira na kuongezeka kwa uwekezaji.