1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Rais wa Ujerumani, Horst Köhler, apinga kubinafishwa usalama wa ndege

24 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCzg

Vyombo vya habari nchini hapa Ujerumani vimeripoti kuwa rais wa Ujerumani Horst Köhler amechukuwa hatua ya kutosaini sheria ya serikali kuhusu idara za usalama wa usafiri wa angani. Serikali kuu ya muungano inayoongozwa na Kansela, Angela Merkel, inataka kubinafsisha kwa kiwango fulani shughuli za usalama wa ndege, mpango ambao unaweza kuwaletea bilioni 1 za Euros. Ikiwa rais Köhler atatupilia mbali kabisa mswada huo wa sheria, basi itakuwa mara ya kwanza kutokea kitu kama hicho wakati huu wa serikali ya muungano ya vyama vya Kristian demokrate na Social demokrate. Wakosoaji wa mpango huo wanasema usalama wa safari za ndege ni jukumu la utawala wa nchi kuweza kuachiliwa mtu mwingine.