1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Rais wa Ujerumani ziarani Amerika ya Kusini

4 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCMT

Rais Horst Köhler wa Ujerumani hii leo ameanza ziara yake rasmi ya kwanza barani Amerika ya Kusini.Ziara hii ya siku 12 itampeleka Paraguay,Brazil na Colombia.Hii ni mara ya kwanza kabisa kwa rais wa Ujerumani kuizuru Paraguay.Köhler amefuatana na tume ya kiuchumi na anatazamiwa kuitumia ziara hii kujadilia masuala ya kijamii na kiuchumi.