1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Rais Yuschchenko wa Ukraine ziarani Ujerumani

8 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCTw

Rais Viktor Yuschchenko wa Ukraine,akiwa ziarani nchini Ujerumani,amekutana na Kansela Angela Merkel mjini Berlin.Wakati wa majadiliano yao, Yuschchenko amesisitiza pendekezo la nchi yake la kutaka kuwa mwanachama katika Umoja wa Ulaya. Kansela Merkel ambae hivi sasa ameshika wadhifa wa urais wa Umoja wa Ulaya amesema,upo uwezekano wa kuwa na uhusiano wa karibu na Umoja wa Ulaya,lakini sio uanachama.