1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Rice amuarifu Merkel juu ya ziara ya Mashariki ya Kati

19 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCZd

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani,Condoleezza Rice amekutana na Kansela wa Ujerumani,Angela Merkel mjini Berlin.Wakati wa mkutano huo Rice alimuarifu Merkel juu ya ziara yake ya hivi karibuni katika Mashariki ya Kati.Wote wawili wamesema maendeleo fulani yamepatikana katika juhudi za kuleta masikilizano ya amani kati ya Waisraeli na Wapalestina.Hapo awali Rice na waziri mwenzake wa Ujerumani,Frank-Walter Steinmeier walitangaza kuwa kundi la kimataifa la pande nne kuhusika na Mashariki ya Kati litakutana Washington mwezi wa Februari.Wajumbe wa pande hizo nne ni kutoka Umoja wa Mataifa, Marekani,Urussi na Umoja wa Ulaya.Inatumainiwa kuwa mkutano huo utasaidia kuanzisha duru mpya ya majadiliano ya amani kati ya Israel na Wapalestina.