1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Sinagogi kuwa la Wayahudi lafunguliwa tena

1 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBTx

Kumefanyika sherehe mjini Berlin kuadhimisha kufunguliwa tena kwa sinagogi kubwa kabisa nchini Ujerumani ambayo ni sehemu ya ibada kwa Mayahudi baada ya kufanyiwa ukarabati mkubwa.

Jengo hilo lilinusurika chupu chupu kuteketezwa katika mashambulizi ya mwaka 1938 yalliokuwa yakijulikana kama Kristallnacht.

Huo ulikuwa ni usiku wakati wafuasi wa Adolf Hitler waliziteketeza nyumba za Mayahudi,biashara zao na shemu za ibada.Zaidi ya wageni 1,000 wakiwemo wahanga walionusurika mauaji ya kuwaangamiza Wayahudi na viongozi wa kisiasa wa Ujerumani walihudhuria hafla hiyo.

Kufunguliwa kwa sinagogi hilo kunakwenda sambamba na kuanza kwa tamasha la Kitamaduni la Wayahudi la kila mwaka katika mji mku huo wa Ujerumani ambalo linahusisha maonyesho kadhaa jukwaani kwenye sinagogi hilo lililokarabatiwa upya.