1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Steinmeier haoni sababu ya kujiuzulu

26 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCXu
Rais Mwai Kibaki wa Kenya
Rais Mwai Kibaki wa KenyaPicha: AP

Waziri wa masuala ya nje wa Ujerumani,Frank-Walter Steinmeier amesema haoni sababu yo yote ile ya kujiuzulu kuhusiana na kesi ya Murat Kurnaz,Mturuki aliezaliwa Ujerumani.Kurnaz alizuiliwa na Marekani katika jela ya Guantanamo Bay akishukiwa kuhusika na ugaidi.Waziri Steinmeier ameliambia gazeti la „Bild“ serikali ya Ujerumani ilijaribu kupata uhuru wa Kurnaz licha ya kwamba alikuwa na pasipoti ya Kituruki na si ya Kijerumani.Steinmeier wakati huo alikuwa katika serikali iliyopita ya kansela wa zamani Gerhard Schroeder.Murat Kurnaz aliachiliwa huru na Marekani Agosti mwaka jana baada ya kuzuiliwa miaka minne bila ya kufikishwa mahakamani.