1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Ugaidi ni kitisho kwa usalama na utulivu

15 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC1j

Waziri wa ndani wa Ujerumani,Wolfgang Schäuble amesema,vitendo vya kigaidi vya makundi ya Kiislamu ni kitisho kikubwa kabisa kwa usalama na utulivu wa nchi.Hiyo ni mada iliyopewa kipaumbele na waziri Schäuble alipotoa ripoti ya Ofisi ya Ulinzi wa Katiba ya mwaka 2006.Amesema,Ujerumani itambue kuwa inakabiliwa na kile alichokiita, “harakati za kigaidi za aina mpya”.Mbali na uwezekano wa kuwepo kitisho cha makundi ya kiislamu,Schäuble vile vile ameeleza wasiwasi wake kuhusu kuongezeka kwa idadi ya mashambulio yanayofanywa na wafuasi wa siasa kali za mrengo wa kulia.Amesema,katika mwaka 2006,uhalifu uliotendwa na makundi ya siasa kali za kulia uliongezeka kwa asilimia 14 kulinganishwa na mwaka mmoja kabla ya hapo.Waziri Schäuble alizungumzia kile alichokieleza kuwa ni “mwenendo wa kutisha” kuona kwamba makundi ya sera kali za kulia yanakubaliwa katika jamii.