1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Ujerumani kusaidia ujenzi mpya wa Iraq

8 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CClc

Mratibu wa serikali ya Ujerumani wa ushirikiano na Marekani Karsten Voigt amesema kwamba Ujerumani itakuwa tayari kusaidia ujenzi mpya nchini Iraq iwapo hali ya usalama itaruhusu.

Pia amesema kwamba Ujerumani na Ulaya zitakuwa tayari kutimiza dhima ya kidiplomasia yenye lengo la kuzishawishi Syria na Iran kukubali kuunga mkono juhudi za kutafuta amani nchini Iraq.

Suala la Iraq litapewa kipau mbele kikubwa kwenye agenda ya Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmeir wakati atakapokutana na Waziri mwenzake wa mambo ya nje wa Marekani Condoleezza Rice mjini Washington leo hii.