1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Ujerumani kutuma ndege za Tonado Afghanistan.

10 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCKj

Wabunge wa bunge la Ujerumani wameidhinisha jana kutumwa kwa ndege sita za upelelezi chapa Tonado nchini Afghanistan , wakikubali ombi la jeshi la NATO kusaidia kuongeza ukusanyaji wa taarifa za kijasusi kabla ya kuanza kwa mashambulizi ya wapiganaji katika majira ya machipuko.

Wabunge katika baraza la wawakilishi , Bundestag, walipiga kura kutuma ndege hizo nchini Afghanistan , pamoja na kiasi cha wafanyakazi 500 na mafundi.

Ujerumani ina kiasi cha wanajeshi 3,000 katika nchi hiyo, hasa katika mji wa Kabul pamoja na maeneo ambayo ni salama zaidi ya kaskazini. Ujerumani imekataa mbinyo kutoka kwa mataifa mengine ya NATO kuweka wanajeshi wake katika maeneo hatari upande wa kusini.