1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Ujerumani kuyataka mataifa ya Afrika kudhibiti fedha zaidi.

19 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC0r

Ujerumani imetoa mpango wa utekelezaji kwa ajili ya kundi la mataifa yenye viwanda duniani ili kuleta utawala bora zaidi wa fedha katika Afrika.

Pendekezo hilo lina lengo la kuweka hali bora kwa ukuaji wa uchumi wa mataifa ya Afrika, maendeleo, na hali endelevu ya muda mrefu.

Ujerumani , ambayo inashikilia urais wa kundi hilo la G8, itajadili pendekezo la utawala bora na mawaziri wa fedha kutoka Afrika pamoja na kundi la G8 katika mkutano ambao utaanza siku ya Ijumaa mjini Potsdam, karibu na Berlin.

Pia katika mkutano huo , waziri wa fedha wa Ujerumani Peer Steinbrück amesema anamatumaini makubaliano yanaweza kufikiwa hivi karibuni ndani ya kundi la G8 kwa kuwa na utaratibu wa kimaadili wa kuwa na mfuko wa fedha wa tahadhari kwa ajili ya viwanda.

Ujerumani imekuwa ikieleza mara kwa mara wasi wasi wake kuhusu hatari ya uthabiti wa masuala ya kifedha kutokana na hifadhi ya fedha za makisio ya tahadhari.