1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Ujerumani na Japan zatoa wito kuendelea vikwazo

11 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCbi

Kansela wa Ujerumani, Bibi Angela Merkel na Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe, wamesema vikwazo vya silaha vilivyowekwa na Umoja wa Ulaya dhidi ya China vinapaswa kuendelea.

Baada ya mkutano kati ya viongozi hao wawili mjini Berrlin, Waziri Mkuu Shinzo Abe aliwaambia waandishi wa habari anachelea hali ya mambo kubadilika katika eneo lake iwapo China itapata fursa ya kujiendeleza kijeshi.

Bibi Merkel alisema serikali yake haina mpango wa kubadilisha msimamo wake kuhusiana na vikwazo hivyo vilivyowekwa dhidi ya China mwaka elfu moja mia tisa na themanini na tisa wakati ilipokabiliana vikali na wanafunzi waliokuwa wakitetea demokrasia.

Shinzo Abe ataendelea na ziara yake leo na hivyo kuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Japan kutembelea makao makuu ya NATO mjini Brussels, Ubelgiji.