1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Ujerumani na Ufaransa kuisadia Marekani

20 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CPay

Ujerumani na Ufaransa zimeanzisha juhudi za kidiplomasia kuhakikisha mkutano kuhusu amani ya Mashariki ya Kati utakaoongozwa na Marekani baadaye mwezi huu, unafaulu.

Ujerumani na Ufaransa zina ushawishi mzuri zaidi miongoni mwa nchi za kiarabu zikilinganishwa na Mrekani. Wachambuzi wanasema ushirikiano huu unaashiria mabadiliko ya hisia kati ya Ulaya na Marekani.

Marekani inauhitaji msaada wa Ulaya ili kufaulu kuutanzua mzozo wa Mashariki ya Kati, huku Ujerumani na Ufaransa zikionyesha msimamo mpya wa kutaka kuisaidia Marekani iondoe sifa mbaya katika maeneo kadhaa ya mizozo.