1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Ujerumani yachunguza ujumbe wa kigaidi ulioko katika video.

12 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCJx

Serikali ya Ujerumani inasema kuwa wataalamu wanachunguza ujumbe uliomo katika kanda mbili za video ambazo zimetolewa katika mtandao wa internet, ambazo huenda ni kutoka kwa magaidi.

Video ya hivi karibuni kabisa inatoa vitisho dhidi ya Ujerumani na Austria vya mashambulizi, hadi pale itakapoondoa majeshi yake huko Afghanistan.

Hii inafuatia video ya kwanza iliyotumwa siku ya Jumamosi ambapo wapiganaji wa Iraq wanaomshikilia mwanamke mmoja Mjerumani na mtoto wake wametishia kuwauwa iwapo Ujerumani haitaondoa majeshi yake kutoka Afghanistan katika muda wa siku kumi. Ujerumani ina wanajeshi 3,000 wanaotumikia jeshi la NATO nchini Afghanistan. Wawakilishi wa serikali ya Ujerumani mjini Berlin wamesema kuwa nchi hii haipaswi kusalim amri kwa wapiganaji hao.