1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin: Ujerumani yaunga mkono Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Darfur.

2 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBcw

Ujerumani imeunga mkono uamuzi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wa kupeleka wanajeshi elfu ishirini na sita wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja huo pamoja na Umoja wa Afrika katika jimbo la Darfur linalokabiliwa na vita nchini Sudan.

Waziri wa mambo ya nje wa Sudan, Lam Akol, pia amesema serikali yake imelidhia azimio hilo.

"Kwa ujumla tunalikubali azimio hilo. Tunatoa ahadi kwamba tutalizingatia kwa dhati azimio lenyewe“

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier aliwaambia waandishi wa habari mjini Abuja, Nigeria kwamba uamuzi wa Umoja wa Afrika kukubali kutekeleza jukumu hilo ni mwelekeo mzuri.

Hata hiyo serikali ya mseto wa vyama inayoongozwa na Kansela Angela Merkel imesema haitapeleka wanajeshi wa ziada katika eneo hilo.

Msemaji wa serikali amesema Ujerumani itadumisha idadi ya askari mia mbili walioko katika eneo hilo wanaoshugulikia uchukuzi wa kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Afrika.

Serikali ya Sudan imeahidi itashirikiana na kikosi hicho cha kulinda amani.